Thursday, November 10, 2016

Martin Kadinda asema Diamond hakukosea kuvaa mavazi aliyovaa kwenye video ya wimbo ‘Salome’

Mbunifu wa mavazi nchini, Martin Kadinda amefunguka kwa kusema kuwa Diamond hakukosea kuvaa mavazi aliyovaa kwenye video yake ya wimbo ‘Salome’ baada ya watu katika mitandao ya kijamii kudai mavazi hayo hayakuendana na uhalisia ya video hiyo.
Rekodi Mpya Kwa Video ya SALOME! ( Tar 2/ 11/ 2016) Ingia hapa Kuiona
Mbunifu huyo ambaye pia amekuwa akimvalisha Diamond Platnumz, amesema hakuona tatizo kwa Diamond kutumia mavazi yale kwa kuwa ni mavazi ambayo yamekuwa yakitumika zaidi Afrika.

PICHA 10 KALI ZA WASANII WALIOSHINDA AFRIMA 2016 – #Chibu

“Mimi nimependa kwa sababu hajavaa nguo kutoka China lakini amevaa nguo za kiafrika kwa sababu sisi sote ni waafrika,” alisema Martin. “Lakini hayo malumbano niliyasikia katika mitandao ya kijamii na sikutaka kuyaingilia kwa sababu mimi naamini kile alichokifanya tayari alikuwa team ambayo ilikuwa inamshauri,”

VIDEO: Diamond Platnumz Alivyoshinda Tuzo 3 Za Afrima2016 ( LAGOS Nigeria ) part 2

Pia mbunifu huyo amewapongeza wasanii kuamua kuwatumia wabunifu mbalimbali katika kazi zao huku akiitaka serikali kuipa nguvu tasnia hiyo ya ubunifu.

Gazeti La Forbes Latoa Orodha ya wanamuziki Matajiri Duniani. Unajua ni nani anayeongoza Barani Afrika? [ Richest Artist in Africa ]

Martin ni mmoja kati ya wabunifu ambao watashiriki kuonyesha mavazi yao katika tamasha kubwa la mavazi nchini, Swahili Fashio Week.

Share on Facebook
Share on Twitter
Share on Google+

Related : Martin Kadinda asema Diamond hakukosea kuvaa mavazi aliyovaa kwenye video ya wimbo ‘Salome’

0 comments:

Post a Comment